Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:28

Museveni huwenda akaanza tena kutia saini adhabu za vifo


Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni

Kiongozi wa Uganda, Yoweri Museveni huenda akaanza tena kutia saini adhabu za vifo baada ya mapumziko ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za kuondoa wimbi la uhalifu, amesema hayo kwenye Twitter.

Maoni ya bwana Museveni haraka yalishutumiwa vikali na wanaharakati wa kutetea haki ambao wanapinga adhabu ya kifo.

Mfano wa kitanda kinachotumika kwa adhabu ya kifo
Mfano wa kitanda kinachotumika kwa adhabu ya kifo

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Reuters kifo bado ni adhabu ya juu nchini Uganda kwa makosa mbali mbali ya uhalifu ikiwemo mauaji, uhaini na ubakaji, lakini hakuna mtu aliyenyongwa tangu mwaka 1999. Msemaji wa huduma za magereza nchini Uganda amesema hivi sasa kuna takriban wafungwa 278 waliohukumiwa kifo.

Katika tweet yake Museveni ambaye amekuwepo madarakani tangu mwaka 1986 amesema amekuwa akisita kutia saini adhabu ya kunyongwa kwa wahalifu kwasababu yeye ni ‘mkristo.’

“Lakini kuwa mpole kunasababisha watu kudhani kwamba wanaweza kufanya uhalifu na kutoadhibiwa. Nitabadili msimamo wangu,” amesema.

Waganda wamekuwa wakilalamika juu ya kuongezeka kwa uhalifu katika miaka ya karibuni hasa kuzunguka mji mkuu Kampala.

Mfululizo wa visa vya kikatili ikiwemo mauaji ya wanawake mwaka jana ambapo miili yao ilitupwa kando ya barabara katika eneo kubwa la kusini mwa Kampala na kuripotiwa kwa kiasi kikubwa katika vyombo vya habari kama ilivyo kwa mashambulizi ya kutumia mapanga wakati wa mwaka mpya ambapo watu watano waliuawa katika eneo la vijijini.

Wakosoaji wa serikali mara kwa mara wanalishutumu jeshi la polisi la nchi hiyo kwa kuelekeza juhudi zao katika kuwasaka wapinzani wa kisiasa wa Museveni badala ya kupambana na uhalifu ambapo idadi ya wale wanaofikishwa mbele ya sheria iko chini mno.

XS
SM
MD
LG