Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 08:07

Museveni 'Hatutadhibiti gharama ya juu ya maisha. kuleni mihogo, mawele'


Rais wa Uganda Yoweri Museveni
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba hawezi kuingilia katika kutatua kupanda kwa bidhaa muhimu nchini humo, akaidai kwamba hatua kama hiyo inaweza kuangusha uchumi wa nchi hiyo.

Wabunge walikuwa wamependekeza kwamba serikali ipunguze ushuru kwa bidhaa muhimu ili kuhakikisha kwamba raia wanapata bidhaa muhimu kwa matumizi ya nyumbani.

“Baadhi ya watu wanafikiria kwamba kuondoa ushuru kwa baadhi ya bidhaa wakati bei yake imepanda ni suluhisho. Unapofanya hivyo kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, unaingiza nchi katika hatari kubwa sana. Uchumi utaanguka,” amesema Museveni katika hotuba ya taifa.

Museveni amesema kwamba hawezi kuagisa kupunguzwa kwa bei ya Petroli.

Bei ya bidhaa muhimu imekuwa ikiongezeka Uganda imesababisha hasiwa na wasiwasi mkubwa. Raia wa Uganda wamekuwa wakitaka serikali kuchukua hatua za haraka kudhibithi ongezeko hilo.

Museveni ameshauri raia wa Uganda kutumia bidhaa zilizozalishwa ndani ya nchi kama mtama, mihogo, ndizi, njugu, nyama, mbaazi na kadhalika badala ya kula wali au mkate.

​
XS
SM
MD
LG