Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:35

Museveni atishia kuingia DRC


Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jumapili ametishia kuingia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kifua mbele kuwasaka waasi wa kikundi cha Allied Democratic Forces, ADF, anaodai wanahusika katika mauaji nchini Uganda.

Rais amezungumza hayo wakati wa maombi maalum ya kuomboleza kifo cha msaidizi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Uganda, Felix Kaweesi huko Kulambiro, nje ya mji wa Kampala na kueleza lengo lake kubwa hivi sasa ni kuwasaka na kuwaua wale anaodai ni wahalifu.

Hivi karibuni watu wasiojulikana waliwapiga risasi na kuwaua maafisa wa jeshi akiwemo kamanda Kaweesi ambae pia alikuwa msemaji wa jeshi hilo.

Taarifa za jeshi la polisi zilisema kuwa mlinzi na dereva wake waliuawa pia katika shambulio hilo,

Kadhalika Rais ametoa agizo kwa maafisa wake wenye silaha bila ya kusita kumpiga risasi mtu yoyote wanaemshuiku kwamba ana silaha na anania ya kuwashambulia.

Museveni pia amedai kuwa baadhi ya polisi ni majambazi na kuwataka polisi kujichunguza kwani ana imani wako ambao wanaua raia.

Amewataka raia walio na taarifa muhimu kuripoti akiwashutumu maafisa wa usalama kuwa hawaaminiki.

Akionekana mwenye hasira, Museveni amesema wale wanaoua watu nchini Uganda kwa kutumia bunduki wakitumia usafiri wa pikipiki ni nguruwe na amesisitiza nguruwe hao watauawa.

Museveni pia ametishia kupunguza idadi ya wahudumu wa boda boda jijini Kampala, akisema wahudumu hao Sasa wanatumika na wahalifu.

Museveni pia amechukua fursa hiyo kuonya watumishi wa umma dhidi ya kudai nyongeza ya mishahara akisema wanaofanya hivyo wanajitafutia matatizo.

Kwake Museveni, mishahara kwa wafanyakazi ndio inayolemaza juhudi zake za kuekeza katika usalama kwani kiasi kikubwa cha Pesa kinatumika kulipa mishahara.

Ameamrisha mamlaka jijini kampala kuweka kamera za CCTV katika jiji lote ili kuwanasa wahalifu kwa haraka, akisema hiyo ndiyo mbinu ya kisasa inayotumika katika Nchi na miji ilioendelea kama New York.

Kwake Museveni, mbinu zinazotumika kukabiliana Na wahalifu nchini Uganda ni za zamani, ikiwa pamoja na kuwauliza walioshuhudia.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennes Bwire, Uganda

XS
SM
MD
LG