Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ametishia kumkamata mpinzani wake katika uchaguzi mkuu wa mwezi Februari Dkt Kiiza Besigye kwa kutoa matamshi anayodai ni mpango wa kuwachochea raia dhidi ya serikali yake na kupanga kumpindua kwa kutumia nguvu za raia.
Rais Museveni amedai kuwa matamshi ya Dkt Besigye ni sawa na njama ya kupindua serikali kwa kutumia nguvu za wananchi. Amesema kuwa uchunguzi na kanda zinafanyawiwa uchunguzi wa kubainisha hatua za kisheria atakayo chukuliwa Bisigye iwapo madai hayo yatadhibitishwa kuwa ya kweli.