Muhammad Ali Pate, Profesa wa chuo cha Harvard nchini Marekani ambaye ameshikilia nafasi za cheo cha juu katika sekta ya afya nchini Nigeria amekataa nafasi katika muungano wa chanjo ya kimataifa ya Gavi, shirika hilo lilitangaza Jumatatu.
Pate, daktari aliyepata mafunzo ya magonjwa jumla na magonjwa ya kuambukiza alitarajiwa kuchukua nafasi hiyo Agosti 3, GAVI ilitangaza mwezi Februari, akichukua nafasi ya daktari wa magonjwa ya kuambukiza kutoka Marekani Seth Berkley, ambaye alikuwa akisimamia kitengo hicho tangu mwaka 2011.
Pate aliifahamisha Gavi kwamba amechukua uamuzi mgumu sana kukubali ombi la kurudi nyumbani na kuendelea kutoa huduma ndani ya nchi yake Nigeria, taarifa hiyo ilisema bila maelezo zaidi kuhusu uamuzi huo.
Afisa Mkuu wa Operesheni za Gavi, David Marlow, badala yake atakaimu nafasi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Muda wakati utafutaji wa Mkurugenzi Mtendaji mpya unaendelea. Muungano wa chanjo ya Gavi, ni shirika lisilo la kiserikali lililoundwa mwaka 2000 kutoa chanjo kwa nchi zinazoendelea.
Forum