Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:36

Mugabe akanusha kufanyiwa upasuaji


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anasema ripoti kwamba alifanyiwa upasuaji huko Malaysia kwa maneno yake ni uongo mtupu uliosambazwa na vyombo vya habari vinavyodhaminiwa na Magharibi.

Rais huyo ambaye anatimiza miaka 87 mwezi ujao, alirudi Harare kutoka safari yake nje ya nchi Jumapili.Katika mahojiano na televisheni ya taifa, bwana Mugabe alisema alikuwa kwenye likizo ya mwaka huko Singapore na alikanusha kwamba alikuwa Malaysia.

Wiki iliyopita, vyanzo vya kidiplomasia huko Zimbabwe na Afrika Kusini vilisema Rais Mugabe alikuwa Malaysia akifanyiwa matibabu ya tatizo la korodani.

Bwana Mugabe alionekana kuwa salama na anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika-AU huko Addis Ababa nchini Ethiopia baadaye wiki hii.
Rais pia alisema Jumapili kwamba kama serikali ya Zimbabwe iliyopo madarakani haikubaliani juu ya katiba mpya, ana haki ya kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya chini ya mfumo wa zamani.

Taratibu za kuandika katiba zipo nyuma ya ratiba kwa miezi kadhaa. Rais Mugabe na chama chake cha ZANU-PF kilitia saini ya mkataba wa kushirikiana madaraka mwaka 2008 na Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai, kiongozi wa chama cha Movement for Democratic Change.

Chini ya vipengele vya mkataba, serikali inaweza kuendelea hadi mwaka 2013. Hata hivyo wengi katika chama cha ZANU-PF wanasema serikali inamaliza maadhimisho ya pili ya muda wake mwezi ujao.

Bwana Mugabe ameitawala Zimbabwe tangu mwaka 1980, wakati nchi ilipopata uhuru kutoka kwa Mwingereza.



XS
SM
MD
LG