Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 18:14

Mugabe awasihi wahamiaji wa Afrika kusini kurudi makwao


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe (L) na Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma wakati Mugabe alipotembelea Afrika kusini April 8, 2015
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe (L) na Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma wakati Mugabe alipotembelea Afrika kusini April 8, 2015

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, jumatano aliwasihi wahamiaji walioshambuliwa nchini Afrika kusini kurejea majumbani mwao. Matamshi yake yalikuja mwishoni mwa mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC unaoangalia namna eneo hilo linavyoweza kujiendesha kiviwanda.

Mwishoni mwa mkutano wa siku moja viongozi kutoka SADC walitoa tamko la pamoja walisema eneo hilo liliridhika na hatua ambayo serikali ya Afrika kusini imechukua kuhakikisha kwamba mashambulizi ya hivi karibuni juu ya wahamiaji hayatatokea tena.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Bwana Mugabe ambaye ni mwenyekiti wa SADC na Umoja wa Afrika aliwaambia waandishi wa habari kwamba hakukuwa na haja kwa wa-Afrika kwenda Afrika kusini, taifa la pili lenye uchumi mkubwa sana katika bara la Afrika. “Watu wetu hawana haja ya kukimbilia nchini Afrika kusini. Wanafikiri Afrika kusini ni peponi kwetu katika eneo la kusini mwa Afrika. Ndio, kuna maendeleo Zaidi. Lakini nenda huko na utaona kwamba wa-Afrika bado wapo chini. Ni wazungu ambao wanaishi maisha bora Zaidi”.

Makadirio yanaonesha kwamba wazimbabwe ndio kundi kubwa sana la wahamiaji walioathirika huko Afrika kusini kutokana na mashambulizi ya wageni. Wanakadiriwa kuwa watu milioni tatu.

Kabla ya kwenda kwenye mkutano huo mjini Harare, Rais wa Afrika kusini, Jacob Zuma alisema alitaka suala hili kujadiliwa japokuwa halikuwemo kwenye ajenda. Rais wa Malawi Peter Mutharika pia alieleza kwamba alitaka SADC kuzungumzia suala la mashambulizi ya wageni.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan

Rais wa Nigeria anayeondoka madarakani, Goodluck Jonathan alimuagiza kaimu balozi wa Nigeria kwa Afrika kusini, kupinga namna Pretoria ilivyoshughulikia mashambulizi ambayo yalidaiwa kusababisha vifo vya watu saba.

Umoja wa Afrika-AU ulisema unakaribisha juhudi za Afrika kusini za kumaliza ghasia lakini kazi zaidi lazima ifanywe ili kuwalinda wa-Afrika na wahamiaji wengine wa kigeni.

XS
SM
MD
LG