Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:47

Muda wa wafuatiliaji waongezwa Syria


Basi la polisi likiwa limeharibiwa na shambulizi la bomu
Basi la polisi likiwa limeharibiwa na shambulizi la bomu

Wanaharakati wa upinzani wa Syria na makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa wafuatiliaji hao

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa nchi za kiarabu wamekubaliana kuongeza muda wa ujumbe wa wafuatiliaji wanaojaribu kufuatilia ukandamizaji unaosababisha mauwaji unaofanywa na serikali ya Syria dhidi ya upinzani wa wananchi unaendelea kwa miezi kumi sasa.

Wanadiplomasia waandamizi kutoka Qatar na mataifa mengine ya kiarabu walikutana Cairo Jumapili na wametoa mwito wa kutaka ujumbe wa ufuatiliaji wa Umoja wa nchi za kiarabu huko Syria uimarishwe na kushinikiza kumalizika kwa ghasia nchini humo.

Ufuatiliaji huo ulianza desemba 26.

Haikufahamika mara moja ni hatua gani zitachukuliwa kuimarisha ujumbe huo ambao una takriban watu 150 huko Syria.

Wanaharakati wa upinzani wa Syria na makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa wafuatiliaji hao na kusema kuwa kuwepo kwao kumeshindwa kuhakikisha kumalizika kwa ukandamizaji unaofanywa na majeshi yanayomtii rais wa Syria Bashar Al Asaad.

Baadhi ya wakosoaji wametoa mwito kwa jumuiya hiyo kuondoa wafuatiliaji hao.

XS
SM
MD
LG