Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:31

Muandamanaji mmoja  wa Sudan auawa baada ya kupigwa risasi


Muandamanaji wa Sudan akiwa ameshikilia bango lenye picha ya muandamanaji anayedaiwa kuuawa na vikosi vya usalama lililoandikwa 'Hakuna ushirikiano, Hakuna usawa.
Muandamanaji wa Sudan akiwa ameshikilia bango lenye picha ya muandamanaji anayedaiwa kuuawa na vikosi vya usalama lililoandikwa 'Hakuna ushirikiano, Hakuna usawa.

Muandamanaji mmoja  wa Sudan aliuawa Jumanne baada ya kupigwa risasi kifuani wakati wa maandamano ya kupinga utawala wa kijeshi, Kamati Kuu ya Madaktari wa Sudan ilisema katika taarifa.

Polisi wa Sudan walisema katika taarifa kwamba ufyatuaji risasi huo ni hatua ya mtu binafsi iliyokwenda kinyume na amri na kwamba taratibu za kisheria zimechukuliwa mara moja dhidi ya polisi aliyehusika.

Mwandamanaji huyo, ambaye aliuawa katika eneo la Sharg al-Nil karibu na mji mkuu wa Sudan, amekuwa mwandamanaji wa 125 kuuwawa katika maandamano ya kila wiki yaliyoanzishwa na mapinduzi Oktoba mwaka 2021.

Waandamanaji walioonekana wakiandamana kuelekea ikulu ya rais mjini Khartoum na jirani ya Omdurman walikutana na mabomu ya machozi kutoka kwa polisi, shahidi wa Reuters alisema.

Maandamano hayo yanakuja huku viongozi wa kijeshi waliochukua madaraka katika mapinduzi hayo wakijadiliana makubaliano na vyama vya kiraia vilivyokuwa madarakani hapo awali ili kurejesha serikali ya kiraia.

XS
SM
MD
LG