Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:03

Mtu mmoja auwawa kwenye shambulizi la bomu Jerusalem.


Eneo la shambulizi la bomu nchini Israel kwenye picha ya maktaba.
Eneo la shambulizi la bomu nchini Israel kwenye picha ya maktaba.

Milipuko miwili imeteguliwa mapema Jumatano karibu na vituo vya mabasi mjini Jerusalem na kuuwa mtu mmoja huku wengine takriban 14 wakiachwa na majeraha kwa kile polisi wametaja kuwa shambulizi linaloshukiwa kutekelezwa na wapalestina.

Ripoti zinaongeza kusema kwamba milipuko hiyo imetokea wakati kukiwa na msongamano mkubwa wa magari huku polisi wakilazimika kufunga sehemu ya barabara kuu kutoka nje ya mji huo, ambako mlipuko wa kwanza ulitokea.

Mlipuko wa pili umetokea kwenye kitongoji cha Ramot, kaskazini mwa mji huo. Matukio hayo yamefanyika wakati hali ya taharuki kati ya Israel na Palestina ikiwa imeongezeka kufuatia miezi kadhaa ya mashambulizi kutoka Israel kwenye sehemu iliyokaliwa ya Ukingo wa magharibi kufuatia mashambulizi kutoka wapalestina, yaliouwa watu 9.

Ripoti ya polisi inasema kwamba kando na mtu aliyekufa kwenye tukio la leo, wengine wanne wameachwa na majeraha mabaya.

XS
SM
MD
LG