Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 02:34

Mtu mmoja akamatwa kwa shambulizi la Mombasa


Mtaa ambao mgahawa wa Club Bella Vista unapatikana Mombasa
Mtaa ambao mgahawa wa Club Bella Vista unapatikana Mombasa

Shambulio hilo la Jumanne usiku katika ukumbi wa Club Bella Vista, lilisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Polisi mjini Mombasa imemkamata mtu mmoja mshukiwa wa ugaidi, anayehusishwa na shambulio la Grunedi katika Mgahawa mmoja maarufu katika mji huo.

Shambulio hilo la Jumanne usiku katika ukumbi wa Club Bella Vista, lilisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Mshukiwa huyo amekuwa akihudumia majeraha aliyopata kutokana na shambulio hilo katika hospitali moja mjini Mombasa na majeruhi wengine watano. Washukiwa wenzake wamefanikiwa kutoroka.

Mtu huyo aliyefariki ni mfanyakazi wa club hiyo ya Bellavista inaripotiwa kuwa watu watatu wenye silaha walivamia mgahawa huo wakiwa na vifaa vya vilipuzi na bunduki.

Baada ya kukaidi amri ya kukaguliwa na walinzi wa mgahawa huo walirusha guruneti na kufyatua risasi kwenye mgahawa huo maarufu kwa kuonyesha michuano ya kandanda ambao huvutia watalii na raia wa Kenya.

Hili ni shambulio la tatu chini ya miezi mitatu mpaka sasa zaidi ya watu 10 wamefariki dunia katika visa tofauti tangu jeshi la Kenya kuingia Somalia katika jitihada za kuwasaka Al shabab.

Akizungumza na Sauiti ya Amerika kiongozi wa jumuiya ya kiislam nchini Kenya shekhe Mohamed Door amesema ni idadi ya kikosi cha polisi ni ndogo sana na lazima serikali iongeze idadi ya Polisi, vituo vya polisi na magari akiongeza hilo si ombi bali ni jukumu lao.

XS
SM
MD
LG