Lucile Randon ambaye pia anajulikana kama sister Andre alizaliwa kwenye mji wa Alews kuisini mwa Ufaransa Februari 11, 1904. Msemaji huyo kwa jina David Tavella amesema pia kwamba Andre ni manusura mkongwe zaidi wa maambukizi ya covid-19 na kwamba amefariki Jumanne akiwa kwenye kituo cha afya cha St Catherine Laboure kilichoko kwenye mji wa Toulon.
Kundi la utafiti la Gerontology ambalo huorodhesha watu wenye umri wa zaidi ya miaka 110 au zaidi limeorodhesha Sister Andra kama mtu mwenye umri mkubwa zaidi ulimwenguni baada ya kifo cha Kane Tanaka kutoka Japan mwaka uliopita akiwa na umri wa miaka 119.