Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 08:06

Mteka nyara wa ndege ya EgyptAir kutambuliwa


Waziri wa mambo ya kigeni wa Cyprus mapema leo ameandika kuhusu kukamatwa huko kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Maafisa wa Cyprus wanasema mtu aliyeteka ndege ya abiria ya Misri na kuilazimisha kutua Cyprus amekamatwa.

Maafisa wa Cyprus wamemtambulisha mwanaume huyo kama Seif Eldin Mustafa lakini bado haijabainika lengo la kuteka nyara ndege hiyo ya kampuni ya EgyptAir.

Watu walioshuhudia wanasema mtu huyo alikuwa akitoa amri kwa mkewe wa zamani anaeishi Cyprus huku wengine wakisema alidai kuvaa mkanda wenye vilipuzi.

Karibu abiria wote 55 waliokuwa kwenye ndege hiyo wameachiliwa. Rais wa Cyprus, Nicos Anastasiades, amesema tukio hilo kwenye ndege iliokuwa imepangwa kuelekea Cairo kutoka Alexandria halihusiani na ugaidi.

XS
SM
MD
LG