Wadadisi wanasema madai hayo yataharibu juhudi za rais huyo kuboresha sifa yake kimataifa.
Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, 80, ametawala koloni hilo la zamani la Uhispania lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu 1979.
Baada ya kushinda muhula wa sita madarakani mwezi Novemba, waangalizi wa mambo walisema rais alionekana kuwa na shauku ya kukemea madai yanayoendelea, ambayo ameyakanusha.
Hili linaweza kuhatarishwa baada ya Mahakama Kuu ya Uhispania kutangaza kumchunguza mtoto wa kiume wa Obiang, Carmelo Ovono Obiang, mkurugenzi wa usalama wa rais, Isaac Nguema Endo, na waziri wa usalama Nicolas Obama Nchama kwa madai ya kuteka na kutesa.