Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 11:52

Mtoto wa Mubarak asema hawakuwa na hatia ya rushwa


Gamal Mubarak mtoto wa rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak.
Gamal Mubarak mtoto wa rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak.

Mtoto  wa  kiume wa rais wa zamani wa Misri alisema Jumanne kwamba yeye na wanafamilia hawakuwa na hatia ya mashtaka ya rushwa.

Mashitaka hayo yaliyotolewa katika mahakama za kimataifa baada ya wasi ya mwaka 2011 nchini humo, baada ya mahakama mwezi uliopita nchini Uswizi na Umoja wa Ulaya kutoa uamuzi unaoiunga mkono familia hiyo.

Tangazo la Gamal Mubarak, mtoto wa rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak, limekuja baada ya miaka mingi ya majaribio ya familia ya rais aliyeondolewa madarakani kurejesha heshima yake wakati ikikabiliwa na kesi nchini Misri na nje ya nchi.

Katika video hiyo ndefu ya dakika 20 iliyotolewa mtandaoni na yenye jina la "Taarifa ya familia ya Mubarak juu ya kuhitimishwa kwa mafanikio ya kesi zote za kimataifa za mahakama," alionyesha masuala ya kisheria ya familia kama yalivyotatuliwa.

Alisema kuwa tangazo hilo lilichochewa na vyombo vya habari kutoa tuhuma za uwongo za ufisadi dhidi ya familia yake, lakini hakueleza jinsi familia hiyo ilivyojilimbikizia mali zake kwa kiasi kikubwa.

XS
SM
MD
LG