Mtoto huo alipigwa risasi tumboni polisi walipokuwa wanatekeleza amri ya watu kutotoka nje ya nyumba zao.
Wakati huohuo Rais Uhuru Kenyatta ameomba msamaha kutokana na jinsi maafisa wa polisi walivyotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wakati wakitekeleza amri ya kusalia majumbani inapotimia saa moja kamili jioni.
Polisi wameshutumiwa kutumia nguvu kuzidi kiasi wakati wakitekeleza amri hiyo, tangu ilipoanza ijumaa wiki iliyopita.
Wametumia gesi ya kutoa machozi, virungu, fimbo na hata kufatua risasi dhidi ya raia.