Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:13

Mtoto wa Gadhafi aapa majeshi kupigana hadi kufa


Mtoto wa kiongozi wa Libya Saif-Al-Islam
Mtoto wa kiongozi wa Libya Saif-Al-Islam

Seif al-Islam Gadhafi ameapa kuwa yeye na wajumbe wengine wa familia hawatajisalimisha na alisema kwamba baba yake yuko salama.


Mmoja kati ya watoto wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya Moammar Gadhafi amekiambia kituo kimoja cha televisheni cha Syria jumatano jana kwamba yuko katika vitongoji vya Tripoli na makamanda watiifu wamemwambia wanajeshi watapigana mpaka kufa.

Seif al-Islam Gadhafi ameapa kuwa yeye na wajumbe wengine wa familia hawatajisalimisha na alisema kwamba baba yake yuko salama.

Alikiambia kituo hicho cha televisheni kinachomuunga mkono Gadhafi cha al-Rai katika ujumbe wa kanda ya sauti kwamba hari ya wapiganaji watiifu iko juu sana.

Maelezo yake yanatofautiana na yale ya kaka yake Saadi aliyekiambia kituo cha televisheni cha al- Arabiya kwamba yuko tayari kufanya majadiliano ya kuunda serikali ya mseto na majeshi yanayompinga Gadhafi ili kuzuiya umwagaji damu.

Saad alisema anazungumza kwa kibali cha baba yake.

XS
SM
MD
LG