Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 09:05

Kenyatta akabiliwa na mtihani mwengine wa kutawala Kenya


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Mwaka huu Uhuru Kenyatta, anakabiliwa na mtihani mwingine wa kutawala Kenya, kwa muhula wa pili na kuendeleza historia ya jina la Kenyatta katika utawala wa Kenya.

Aliongeza idadi ya watoto wa marais wa zamani waliofanikiwa kutawala kama baba zao, mnamo Aprili 9 mwaka 2013. Hili si jambo geni duniani kwa sasa. Nchi mbalimbali duniani zimeshatawaliwa na baba na mtoto kwa vipindi tofauti.

Safari yake ya kisiasa ilianzia mwaka 2001 alipochaguliwa kuwa mbunge, na kuteuliwa kuwa waziri wa serikali za mitaa na rais Daniel Arap Moi. Toka alipokuwa mstari wa mbele katika siasa, wengi humuona na kumchukulia kama kijana fulani. Lakini nguvu yake kisiasa, ilikuwa zaidi katika uchaguzi wa Desemba 2002. Chama kikongwe cha KANU kilimpa ridhaa ya kuwa mgombea wake wa urais. Haikuwa rahisi kutokana na upinzani uliojitokeza wa mwanachama wa zamani wa KANU Mwai Kibaki, aliposhinda na huu ukawa mwisho wa nguvu ya KANU. Kenyatta akawa kiongozirasmi wa upinzani ndani ya bunge.

Wchambuzi wengi wanasema, uamuzi wa kumuunga mkono Mwai Kibaki katika uchaguzi wa mwaka 2007, ndiyo iliyokuwa njia njema ya urais wa Kenyatta. Kwa mara nyingine tena akateuliwa kuongoza wizara mbalimbali, na kuongeza ushawishi wake wakisiasa, licha ya safari hii ikiwa nje ya chama cha KANU. Akiwa bado kiongozi wa KANU alijiunga na chama cha Liberal Democratic Party, na kuunda vuguvugu la Chungwa katika kupigania katiba ya Kenya. Uchaguzi uliokuwa na utata wa mwaka 2007, alikiunganisha chama chake na rais Mwai Kibaki dhidi ya mgombea Raila Odinga.

Huu utakuwa muhula wake wa pili na mwisho kama rais wanne wa Kenya. Kwa sasa si KANU tena ama vyama vingine vilivyopita, sasa ni Jubilee. Lakini Uhuru Kenyatta anaingia katika uchaguzi akiwa tayari amesafishwa na mashitaka yake ya ICC. Mwendesha mashitaka wa wakati huo wa mahakama ya The Hague, Luis Moreno Ocampo, alimshtaki kwauchochezi wa ghasia za Kenya za mwaka 2007 baada ya uchaguzi. Kusafishwa huku si kwake tu, bali pia na makamu wake wa rais William Rutto, ambaye sasa ni mgombea wake mwenza katika uchaguzi huu.

Licha ya kuwa na muonekano wa ujana, Uhuru Kenyatta, anaingia katika uchaguzi akiwa na miaka 55. Nyuma yake yupo mke wake wa takriban miaka 26, Margaret Gakuo, aliyebahatika kupata naye watoto watatu. Kenyatta amesomea taaluma za uchumi, sayansi ya siasa na mambo ya serikali katika chuo cha Amherst College nchini Marekani. Anaelezwa kupendelea muziki wa Reggae na ucheshi. Mgombea huyo wa Jubilee ameshawahi kuonekana katika kipindi cha televisheni cha Churchil Show, akifanya ucheshi na kuimba muziki wa Raggae.

XS
SM
MD
LG