Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 13:14

Mteule wa Rais Trump ahojiwa na Baraza la Seneti


Mike Pompeo

Mteule wa Rais Donald Trump katika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje, Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi ya Marekani (CIA), anahojiwa Alhamisi na kamati ya Seneti ikiwa ni hatua ya kuthibitishwa kwake, ambapo ataweka mkazo juu ya msimamo mkali dhidi ya Russia.

“Russia imeendeleza uchokozi, fursa walioichukua kutokana na kuwepo sera dhaifu dhidi ya uchokozi huo. Hiyo ni mwisho sasa,” Pompeo ataiambia kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Baraza la Seneti, kwa mujibu wa nukuu za ushuhuda wake.

Korea Kaskazini na Iran zinategemewa kuwa ni sehemu ya mazungumzo hayo Alhamisi.

Kutofautiana kati ya Rais Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani Rex Tillerson kulipelekea kufukuzwa kwa waziri huyo mwezi Machi.

Lakini Stephen Pompeo wa Kikundi cha Kukabiliana na Migogoro ya Kimataifa anasema iwapo atathibitishwa, Pompeo hatokabiliwa na vipingamizi alivyovikabili Tillerson.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG