Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:43

Mtetemeko wa ardhi wasababisha maafa Uturuki


Mtetemeko wa ardhi wasababisha maafa Uturuki
Mtetemeko wa ardhi wasababisha maafa Uturuki

Video iliyochukuliwa muda mfupi baada ya mtetemeko wa ardhi Uturuki

Mtetemeko mkubwa wa ardhi umetikisa maeneo ya kusini mashariki ya Uturuki karibu na mpaka na Iran siku ya Jumapili asubuhi na kusababisha maafa makubwa.

Mtetemeko huo ulokua na nguvu za 7.2, umesababisha majengo kuporomoka katika eneo hilo la mbali na la watu maskini na inahofiwa idadi ya majeruhi itaongezeka.

Juhudi kubwa za uwokozi zinaendelea wakati watu wanawatafuta walonusurika wakitumia kila kitu walichopata kufukuwa katika vifusi vya nyumba zilizoanguka. Takriban watu 138 wamefariki kutokana na mtetemeko huo.

Mtetemeko mkubwa kabisa ulotokea 1999 huko Istanbul ulisababisha vifo vya takriban watu 20, 000.

Video ya wakati tetemeko lilipokua linatokea

XS
SM
MD
LG