Mtaalamu asiyefungamana na upande wowote anaonya kwamba machafuko mengi yanayoikabili Mali, yanayochochewa na kuongezeka kwa mashambulizi kutoka kwenye makundi yenye silaha ya Kiislamu, yanasababisha kuzorota kwa kasi kwa hali ya usalama wa nchi hiyo, na kukithiri kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, huku kukiwa na madhara makubwa katika eneo hilo.
Ninasisitiza wasiwasi wangu mkubwa kutokana na kuzorota kwa kasi na kuendelea kwa hali ya usalama katika takriban mikoa yote ya Mali ambayo inaonekana kutoka kwenye udhibiti wote wa mamlaka, alisema Alioune Tine, mtaalam huru wa haki za binadamu nchini Mali alisema.
Tine, ambaye aliwasilisha ripoti yake ya hivi karibuni kwenye Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa Alhamisi, alisema "tunazidi kuona makabiliano ya makundi yenye itikadi kali yanayotaka kudhibiti nchi kwa madhara ya raia, ambao ni waathiriwa wakuu walionaswa katika mapigano hayo.
Forum