Upatikanaji viungo

Breaking News

Jopo la madaktari nchini India limekubali kutoa mimba ya msichana wa umri wa miaka 10, ambaye ni muathiriwa wa ubakaji baada ya mahakama kuamuru hatua hiyo ichukuliwe.

Msichana huyo anatoka mji wa Rohtak, jimbo la Haryana, kaskazini mwa nchi hiyo.

Dk Ashok Chauhan ameviambia vyombo vya habari kuwa hatua hiyo sasa inaweza kuchukuliwa wakati wowote.

Mamlaka nchini India zimesema msichana huyo alipata ujauzito karibu miezi mitano iliyopita baada ya kubakwa na baba wa kambo, kitendo kinachoaminika kufanyika mara kadhaa.

Kwa mujibu wa gazeti la India Times, polisi wamesema kuwa mtu huyo tayari amekamatwa.

Sheria nchini India haziruhusu utoaji mimba kwa wanawake wajawazito baada ya wiki 20 bila ya idhini ya madaktari.

Inahofiwa kwamba hatua kama hiyo inaweka maisha ya mwanamke hatarini.

Mahakama moja nchini India iliamuru kwamba madaktari wanaweza kutoa mimba ya msichana huyo.

Kupata mimba kwa msichana huyo kumezua hisia mbali mbali hususan kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watu wakitaka babake wa kambo anyetuhumiwa kumbaka achukuliwe hatua kali za kisheria.

  • 16x9 Image

    BMJ Muriithi

    BMJ Muriithi is an international Broadcaster/ Multimedia specialist with Voice of America (VOA) based in Washington DC. He is a versatile journalist who has, among other assignments, covered major international events, including the UN General Assembly (UNGA) in New York, US, and the African Union Summit in Addis Ababa, Ethiopia. He also covers everyday human interest stories from around the world.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG