Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:16

Mshukiwa wa shambulio kwenye kituo cha treni cha New York akamatwa na kushtakiwa ugaidi.


Picha ya mshukiwa wa shambulio kwenye kituo cha treni cha New York Franck James, mwenye umri wa miaka 62 iliyotolewa na idara ya polisi ya jiji hilo. April 12, 2022. Picha ya AP.
Picha ya mshukiwa wa shambulio kwenye kituo cha treni cha New York Franck James, mwenye umri wa miaka 62 iliyotolewa na idara ya polisi ya jiji hilo. April 12, 2022. Picha ya AP.

Mshukiwa wa shambulio la kufyatulia risasi watu wengi Jumanne kwenye kituo cha treni cha jijini New York amekamatwa Jumatano alasiri na kushtakiwa kwa kosa la ugaidi, wakili wa wilaya ya mashariki ya New York, Breon Peace amewambia waandishi wa habari.

Frank James, mwenye umri wa miaka 62 alikamatwa katika kitongoji cha mtaa wa Manhattan baada ya polisi kupewa kidokezo. Kulingana na gazeti la New York Times, mshukiwa aliwekwa kizuizini bila tatizo.

“Ndugu zangu wakazi wa New York, tumemkamata,” Meya wa jiji la New York Eric Adams amesema.

Inadaiwa kwamba James alitega bomu la moshi kwenye kituo hicho cha treni na kisha akawafyatulia risasi abiriya wakati treni ilipokaribia kituo cha barabara ya 36 katika mtaa wa Brooklyn.

Watu kumi walipigwa risasi, watano wakiripotiwa kujeruhiwa vikali lakini hali yao haiko hatarini. Wote wanatarajiwa kunusurika.

Sababu za shambulio hilo hazijulikani, lakini video zilizowekwa kwenye kurasa za mtandao wa kijamii za James, zinaonyesha kwamba alikuwa mtu mwenye hasira kuhusu mambo mengi.

XS
SM
MD
LG