Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 00:04

Abdeslam afikishwa mahakamani Paris


Salah Abdeslam mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Paris ya Novemba 2015
Salah Abdeslam mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Paris ya Novemba 2015

Mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya Paris, Salah Abdeslam, amefikishwa mbele ya mahakama moja mjini Paris saa chache baada ya kusafirishwa kutoka Ubelgiji.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyekua anaishi Brussels alikua mafichoni tangu mashamblizi ya mabomu ya Novemba 13 katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris.

Alikamatwa mwezi uliyopita siku chache tu kabla ya mashambulizi ya mabomu ya Brussels ya Machi 22 ambayo yanaonekana yana uhusiano na mashambulizi ya Paris. Kundi la Islamic State limedai kuhusika na mashambulizi hayo yote.

Waziri wa sheria wa Ufaransa, Jean Jacque Urvoas, amesema Abdeslam atawekwa kwenye chumba cha peke yake kwenye jela ambalo linaweka wafiungwa wanaoaminika kuwa ni hatari.

Wakili wa Abdeslam, Frank Berton anasema mteja wake "hatokaa kimya anataka kueleza kila kitu na ninadhani anataka kushirikiana na mahakama ya Ufaransa"

Inaamini9ka Abdeslam alikua na jukumu kubwa la uchukuzi katika mashambulizi ya Paris, ikiwa ni pamoja na kuajiri magari na angalau kukodisha nyumba moja ya kuwaficha washambulizi.

XS
SM
MD
LG