Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:49

Mshukiwa mmoja katika shambulizi la Ufaransa bado anatafutwa


Waombolezaji wakishikilia kadi za "I am Charlie" katika dakika za kukaa kimya kuwakumbuka waathirika wa jarida la Charlie Hebdo, Jan. 8, 2015.
Waombolezaji wakishikilia kadi za "I am Charlie" katika dakika za kukaa kimya kuwakumbuka waathirika wa jarida la Charlie Hebdo, Jan. 8, 2015.

Wachunguzi wa mauaji yaliyotokea jumatano kwenye ofisi za jarida moja la Charlie Hebdo nchini Ufaransa walisema mtu mmoja kati ya watu wawili wenye silaha bado hajapatikana ambaye alipata mafunzo ya ugaidi kutoka kundi lenye uhusiano na al-Qaida nchini Yemen.

Walisema Said Kouachi alikaa miezi kadhaa nchini Yemen mwaka 2011, lakini hakuna ushahidi kamili kwamba Kouacho na mtu mwingine mwenye silaha anayetafutwa, ambaye ni mdogo wake wa kiume aitwae Cherif walipewa maagizo na kundi lolote la gaidi.

Ndugu hao wote walifahamika na maafisa wa ugaidi wa Marekani na Ufaransa. Cherif alifungwa jela nchini Ufaransa kwa kujaribu kusafiri kwenda Iraq. Walikuwa kwenye orodha ya serikali kuu ya Marekani ya washukiwa ugaidi na pia kwenye orodha ya kutosafiri katika anga ya Marekani.

Zaidi ya polisi na majeshi ya usalama 88,000 wanawatafuta ndugu hao. Mshukiwa wa tatu, Hamyd Mourad mwenye umri wa miaka 18 alijisalimisha alhamis baada ya siku moja ya msako mkali katika eneo.

Waombolezaji mbele ya ubalozi wa Ufaransa huko Copenhagen, Jan. 8, 2015.
Waombolezaji mbele ya ubalozi wa Ufaransa huko Copenhagen, Jan. 8, 2015.

Wakati huo huo, dunia inaomboleza vifo vya watu 12 waliouwawa katika mauaji ya siku ya jumatano kwenye ofisi za jarida hilo linalochapisha picha za katuni na linalojulikana kwa kuzidhihaki dini zote ikiwemo uislam. Polisi wawili ni miongoni mwa waliokufa.

Wa-Faransa walisimama kimya siku ya alhamis katika hali ya hewa ya baridi na mvua wakishikilia kalamu na penseli kama ishara ya haki ya uhuru wa kuzungumza. Taa za jengo la Eiffel Tower zilipunguza mwangaza alhamis usiku ili kutoa heshima kwa waathirika.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilikaa kimya kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanza kikao chake cha alhamis.

Rais wa Marekani Barack Obama alitia saini kitabu cha maombolezo kwenye ubalozi wa Ufaransa mjini Washington. Aliyaita mauaji hayo ya ukatili na kishetani.

Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder
Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder

Wakati huo huo mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder atasafiri kuelekea Paris nchini Ufaransa siku ya jumapili baada ya waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve kuitisha mkutano wa kuzungumzia mashambulizi ya ugaidi na msimamo mkali.

Jarida la Charlie Heblo lilisema litachapisha nakala milioni moja katika tolea lijalo la Januari 14 mwaka 2015.

XS
SM
MD
LG