Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 05:09

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya Rwanda aaga dunia


KanaliTheoneste Bagosora akiwa mbele ya mahakama ya kimataifa kuhusu Rwanda , Arusha , Tanzania mwaka wa 2005

Theoneste Bagosora ambaye alikuwa wakati mmoja kanali wa jeshi  na ambaye anasemekana kuwa mshukiwa mkuu katika kupanga mauaji ya kimbari ya 1994 chini Rwanda ameaga dunia Jumapili akiwa na umri wa miaka 80.

Bagosora alikuwa akitumikia kufungo cha miaka 35 jela, baada ya kupatikana na hatia ya ukatili wa kibinadamu na mahakama maalum ya kimataifa iliyobuniwa kwa ajili ya Rwanda.

Mwanzoni mwaka wa 2008, Bagosora alihukumiwa kifungo cha maisha lakini baada ya kukata rufaa, kufungo hicho kikapunguzwa hadi miaka 35 jela. Wakati akiwa mfuasi sugu wa chama cha National Republican Movement for Democracy and Development chake rais aliyeuawa Juvenal Habyarimana, Basogora mwaka wa 1993 alichaguliwa kuwa waziri wa ulinzi wakati akishika udhibiti wa kitaifa wa jeshi pamoja na masuala ya siasa.


Baada ya Habyarimana kufa kwenye ajali ya ndege, Bagosora alichukua udhibiti wa taifa wakati akiamuru kuuawa kwa wa Tutsi kulingana na manusura wa mauaji hayo Donat Rutayisire wakati akizungumza na shirika la habari la AP. Gen Romeo Dallaire kutoka Canada, ambaye wakati huo alikuwa kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda anamuelezea Basogora kama kiongozi wa mauaji hayo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG