Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:49

Mshukiwa katika shambulizi la ndege ya Lockerbie, raia wa Libya afikishwa mahakamani Marekani


Ndege ta Pan Am 103 iliyoangushwa Lockerbie, Scotland, mwaka 1988
Ndege ta Pan Am 103 iliyoangushwa Lockerbie, Scotland, mwaka 1988

Afisa wa ujasusi wa Libya anayeshutumiwa kutengeneza bomu lililotumika kuiangusha ndege ya Pan Am na kuua watu 259, waliokuwa ndani ya ndege na 11 wakiwa chini, huko Lockerbie, Scotland, amefikishwa mahakamani mjini Washington, Marekani.

Abu Agila Mohammad Masud Kheir Al-Marimi, anashutumiwa kwa uhalifu huo wa mwaka 1988 ambao umetajwa kuwa tukio la kigaidi la kimataifa.

Wizara ya sheria ya Marekani ilitangaza Jumapili kwamba Masud alikuwa amekamatwa, miaka miwili baada ya kufunguliwa mashtaka yanayohusiana na shambulizi hilo.

Maafisa wengine wa ujasusi wa Libya wamefunguliwa mashtaka nchini Marekani kwa kushiriki katika tukio hilo lakini Masud amekuwa wa kwanza kufikishwa katika mahakama ya Marekani kuhusiana na kesi hiyo.

Ndege iliyokuwa inaelekea New York, ililipuka chini ya saa moja baada ya kupaa kutoka London, Desemba 21, 1988. Ilikuwa imebeba raia kutoka nchi 21, waliofariki. Miongoni mwao walikuwa Wamarekani 190.

XS
SM
MD
LG