Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 20:25

Mshtakiwa wa ugaidi afikishwa mahakamani


Ahmed Ghailani, mshukiwa wa mabomu ya ubalozi wa marekani Dar es Salaam

Jaji mmoja wa Marekani amesema mtuhumiwa ulipuaji mabomu Tanzania na Kenya mwaka 1998 Ahmed Khalfan Ghailan, raia wa Tanzania, ana akili timamu kuweza kusimama kizimbani mjini New York.

Jaji wa mmoja wa Marekani, Lewis Kaplan, aliamua Alhamisi kuwa kesi ya Ahmed Khalfan Ghailan, mtanzania ambaye anasubiri kusomewa mashtaka katika mahakama ya kiraia mjini New York, inaweza kuendelea kwa sababu mshitakiwa huyo ana akili timamu. Ghailan anakabiliwa na mashtaka ya ulipuaji wa mabomu mwaka 1998 katika balozi za Kenya na Tanzania ambapo watu 224 wakiwemo wamarekani 12 waliuawa.

Mwanasaikolojia mmoja aliyemwangalia Ghailan alisema wiki kadhaa zilizopita kwamba Ghailani anasumbuliwa na matatizo ya akili kutokana na matibabu aliyopata wakati alipokuwa katika jela ya kijasusi kufuatia kukamatwa kwake mwaka 2004. Ghailani atakuwa mfungwa wa kwanza kutoka Guantanamo Bay kufikishwa katika mahakama ya kiraia hapa Marekani.

XS
SM
MD
LG