Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 21:26

Msako wa kitaifa waendelea Ethiopia


Waziri mkuu wa Ehiopia Abiy Ahmed.

Maafisa wa usalama wa Ethiopia wanaendelea na msako wa kitaifa ambao umepelekea kukamatwa kwa zaidi ya watu 4,500 kwenye eneo moja la taifa kulingana na shirika la habari la AP.

Taarifa zinaongeza kusema kwamba msako huo dhidi ya waandishi wa habari pamoja na wanaharakati ulianzishwa baada ya serikali ya waziri mkuu Abiy Ahmed kutangaza Mei 20 kwamba kuna umuhimu wa kuwalinda wananchi ili kuhakikisha uthabiti wa taifa.

Mapema Jumatatu, maafisa wa usalama kutoka kaskazini magharibi mwa jimbo la Amhara wamesema kuwa zaidi ya watu 4,500 wamekamatwa. Kiongozi wa amani na usalama wa eneo hilo Desalegn Tassew ameambia chombo cha habari cha serikali kwamba ukamataji huo umefanywa ili kuhakikisha kwamba sheria inafuatwa pamoja na kukabiliana na wahuni na kuondoa adui wa kigeni walioko miongoni mwa wakazi. Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binadamu yamelalamikia operesheni hiyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG