Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 10:03

Wanachama wa MRC wasema kukamatwa kwao ni unyanyasaji.


Wanachama wa MRC.
Wanachama wa MRC.

Jeshi la polisi nchini Kenya bado linaendeleza operesheni yake dhidi ya wanachama wa kundi la Mombasa Republican Council maarufu kama MRC licha ya mahakama kuu mjini Mombasa kuamrisha kuwa siyo kundi haramu.

Polisi ya Kenya inadai kuwa kundi hilo ambalo linapigania kujitenga na Kenya na eneo la Pwani ni hatari na linatishia usalama wa eneo la Pwani na taifa kwa jumla.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:04 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Juma lililopita wakati maelfu ya raia nchini humo wakisubiri kuukaribisha mwaka 2016 jumla ya wafuasi 42 wa MRC walitiwa mbaroni tarehe 31 Disemba 2015 katika eneo moja la kusini mwa Pwani ya Kenya walipokua wakifanya mkutano wao.

Kupitia wakili wao Yusuf Abubakar, wanachama wa vuguvugu hilo wametaja hatua ya polisi kuwatia mbaroni kuwa unyanyasaji na kwamba serikali ya Kenya haijatangaza kuwa kundi hilo ni haramu katika gazeti rasmi la serikali.

Kukamatwa kwa watu hao 42 wakiwemo wanawake 7 na wanaume 35 pamoja na kiongozi wao Hamadi Hassan Mwatando mwenye umri wa miaka 79 kulifanyika baada ya kamishna wa kaunti ya Kwale Evans Achoki kuapa kukabiliana na kundi hilo.

Wafuasi wa MRC wakiongozwa na mwenyekiti wao Omar Mwamnuadzi wanakabiliwa na mashitaka mbali mbali katika mahakama za Kenya ikiwemo Mombasa, Kwale na Malindi.

Kwa sasa hatima ya watu hao 42 ikiwa wataachiliwa kwa dhamana Ijumaa tarehe 8 mwezi huu haijulikani.

Vuguvugu la MRC limekua na msukumo wakutaka kujitenga kutoka na Kenya serikali ya Kenya kwa kuifanya pwani ya Kenya kuwa taifa la kujitegemea.

XS
SM
MD
LG