Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:22

Chama cha MPLA chashinda uchaguzi mkuu Angola


Rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos na mkewe Ana Paula katika mji mkuu Luanda
Rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos na mkewe Ana Paula katika mji mkuu Luanda

Kati ya asilimia 85 ya kura zilizohesabiwa, MPLA kilipata robo tatu ya kura zilizopigwa ikifuatiwa na UNITA asilimia 18 na Casa asilimia tano

Vyombo vya habari vya serikali ya Angola vinasema chama tawala cha Rais Eduardo Dos Santos kimeshinda katika uchaguzi mkuu nchini humo.

Tume ya uchaguzi nchini Angola imesema katika asilimia 85 ya kura zilizohesabiwa, chama cha bwana Dos Santos cha Popular Movement for the Liberation of Angola-MPLA - kilikuwa na takribani robo tatu ya kura zilizopigwa.

Chama kikuu cha upinzani cha UNITA kilikuwa na asilimia 18 ya kura. Chama kipya cha upinzani cha Casa kilikuwa na takribani asilimia tano.

Wa-Angola walipiga kura kuchagua wabunge 220 katika bunge. Mkuu wa chama kinachoshinda viti vingi kwa kawaida anakuwa rais mteule.

Bwana Dos Santos na chama cha MPLA wametawala Angola kwa muda wa miaka 32 iliyopita. Taifa hilo limeingia kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika katika muda wa kipindi hicho, lakini watu wake wapatao milioni 19 wanaishi katika hali ya umaskini.
XS
SM
MD
LG