Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:28

Mpinzani wa Senegal aachiwa huru


Sehemu ya ghasia zilizotokana na kukamatwa kwa mwanasiasa wa upinzani Ousmane Sonko, ambaye ameachiliwa kwa dhamana Machi,8, 2021.
Sehemu ya ghasia zilizotokana na kukamatwa kwa mwanasiasa wa upinzani Ousmane Sonko, ambaye ameachiliwa kwa dhamana Machi,8, 2021.

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, ameshtakiwa na kuachiliwa kwa dhamana Jumatatu chini ya usimamizi wa mahakama.

Wakili wake amesema, mwanasiasa huyo anakabiliwa na shutuma za ubakaji zilizochochea maandamano ambayo yaligeuka ghasia.

Kuachiliwa kwa Sonko kunaweza kupunguza mivutano iliyotikisa wiki iliyopita, moja ya taifa la Afrika magharibi ambalo ni tulivu na lenye demokrasia.

Maandamano yalisababisha vifo vya watu wanane katika mapambano kati ya waandamanaji na polisi, shirika la haki za binadamu Amnesty International limesema jana.

Mamia ya watu walikusanyika nje ya jengo la mahakama wakipeperusha bendera na kuimba “ muachie huru Sonko” Jumatatu asubuhi kabla ya kuanza kuandamana.

Wafuasi wake wameitisha mandamano ya kitaifa ya siku tatu wiki hii.

Sonko ambae alipata nafasi ya tatu katika uchaguzi wa rais wa 2019, alikamatwa baada ya mfanyakazi katika saluni ya vipodozi kumshtumu kuwa alimbaka.

Amekanusha madai hayo na kusema kwamba ni njama ya rais wa Senegal, Macky Sall, ya kumuangusha mpinzani wake wa kisiasa.

Serekali ya Senegal imekanusha madai hayo kwamba kukamatwa kwa Sonko ni hila za kisiasa.

XS
SM
MD
LG