Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 15:09

Mpatanishi wa amani aelezea matumaini chanya kwa libya


Mpatanishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Bernardino Leon (C) akiwa na wajumbe wenzake huko Geneva.
Mpatanishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Bernardino Leon (C) akiwa na wajumbe wenzake huko Geneva.

Wakati duru mpya ya mazungumzo ya amani nchini Libya inaendelea, mpatanishi mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema anaamini inawezekana kupata makubaliano ya mwisho ya serikali ya muungano kwa taifa hilo lililokumbwa na mizozo ifikapo mapema mwezi September.

Baada ya miezi ya majadiliano magumu, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Libya, Bernardino Leon, alisema anaona matumaini. Alisema maendeleo mengi yamepatikana katika kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya muungano.

Libya imegawanyika vikali baina ya serikali inayotambulika kimataifa katika mji wa mashariki wa Tobruk, na serikali ya kiislamu iliyopo mjini Tripoli. Taifa hilo lilikumbwa na ghasia tangu dikteta wa zamani Muammar Ghadaffi kupinduliwa hapo mwaka 2011.

Wapiganaji wa kundi la Libya Dawn
Wapiganaji wa kundi la Libya Dawn

Baadhi ya pande katika mzozo huo zilitia saini makubaliano ya amani July 11. Bwana Leon alisema ataendeleza mafanikio hayo kwa kulenga katika kuzishawishi pande ziliosalia kusaini makubaliano ya serikali ya muungano katika duru zake za mazungumzo.

Alisema ishara moja nzuri ni kwamba makubaliano hayo yanaweza kufikiwa katika kipindi cha wiki tatu zijazo ni kuwa wanachama wa pande zinazozozana wamekuja Geneva na wanashiriki katika duru hii ya majadiliano.

“Hili litategemea sana juu ya rai ya kisiasa na hekima na mbinu za pande zote kuleta majina mazuri kwenye meza na mapendekezo mazuri. Kwa hiyo ikiwa hili linawezekana, basi makubaliano na kura ya mwisho na kutiwa saini kwa makubaliano yatafanyika katika wiki za kwanza za mwezi Septemba ili hatima ya mwisho ya utaratibu huu unaweza kupatikana kabla kufanyika mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.”

Bernardino Leon akizungumza huko Geneva, Switzerland, Aug. 11, 2015.
Bernardino Leon akizungumza huko Geneva, Switzerland, Aug. 11, 2015.

Bwana Leon alitambua kuwa hali hii huwenda isipatikane, lakini anaaamnini kuwa kila mtu sasa analiunga mkono na wanataka hili lifanyike. Alisema kuna sababu nyingi kwa pande zinazozozana kuja pamoja hatimaye na kukubaliana juu ya amani. “Kile Libya inakabilwa nacho sasa ni ghasia na mgawanyiko wa nchi. Kwa hivyo ninatumai wahusika wote wa Libya watakuwa na busara kujaribu kuzuia hali kama hiyo na kuharakisha mazungumzo ili kupatikane makubaliano haraka. Nadhani ni hatari kufikia mwezi wa October bila kuwa na makubaliano kwa sababu tutakuwa katika hali tete zaidi.”

Leon alisema upande wa kisiasa wa majadiliano uko mbele zaidi kuliko upande wa usalama. Alisema anapanga kuwakusanya wanajeshi na wanamgambo kwenye meza ya majadiliano. Alisema ni muhimu kuwa na usaidizi wa kijeshi na kuwa na hatua za kuweka mipango ya usalama kama mpangilio wa mwisho wa makubaliano.

XS
SM
MD
LG