Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:31

Mpangilio mpya wa dunia? Utandawazi watikiswa na vita na janga la Corona

FILE -Wakazi wakiwa wamebeba maji kutoka katika ghala la chakula, katika eneo ambalo linadhibitiwa na serikali ya Jamhuri ya Watu wa Donetsk, nje ya mji wa Mariupol, Ukraine, Ijumaa, March 18, 2022. (AP Photo/Alexei Alexandrov)

Uvamizi wa Russia nchini Ukraine umeongeza hofu kuhusu machafuko zaidi, huku kila kitu kuanzia usambazaji wa nishati mpaka vipuli vya mashine hadi uuzaji nje wa ngano na mali ghafi ukiwa hatarini.

Utandawazi, ambao una mashabiki kama ulivyo na wapinzani, uko katika majaribio kuliko wakati wowote mwengine baada ya kipigo mara mbili cha COVID na vita.

Janga lilikuwa tayari limeibua masuali kadhaa kuhusu utegemezi wa ulimwengu kwa kutumia kigezo cha uchumi ambacho kilivunja vikwazo vya kibiashara lakini ulizifanya nchi kutegemeana wakati uzalishaji ulikuwa umesambazwa kwa miongo kadhaa.

Makampuni yamekuwa yakihangaika kukabiliana na vikwazo vikuu katika mfumo wa usambazaji bidhaa duniani.

Uvamizi wa Russia nchini Ukraine umeongeza hofu kuhusu machafuko zaidi, huku kila kitu kuanzia usambazaji wa nishati mpaka vipuli vya mashine hadi uuzaji nje wa ngano na mali ghafi ukiwa hatarini.

Watu wakikimbia vita Ukraine wanangojea basi kuvuka mpaka kwenda Medyka, Poland, Ijumaa, Machi 4, 2022. (AP Photo/Markus Schreiber)
Watu wakikimbia vita Ukraine wanangojea basi kuvuka mpaka kwenda Medyka, Poland, Ijumaa, Machi 4, 2022. (AP Photo/Markus Schreiber)

Larry Fink, mkuu wa kampuni kubwa ya fedha BlackRock, anaeleza wazi wazi: “Uvamizi wa Russia nchini Ukraine umeleta mwisho wa utandawazi ule tuliokuwa tunauelewa kwa zaidi ya miongo mitatu iliyopita.

“Tayari tulikuwa tumeona muingiliano kati ya mataifa, makampuni na pia watu waliokuwa wamebanwa na miaka miwili ya janga la corona,” Fink ameandika katika barua yake kwa wanahisa Alhamisi.

Lakini Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen hakubaliani naye.

“Kwa hakika ni lazima nilikatae hilo,” amekiambia kituo cha televisheni cha CNBC katika mahojiano.

“Tumehusika kwa undani zaidi katika uchumi wa kimataifa. Natarajia hilo litaendelea, ni kitu ambacho kimeleta manufaa makubwa kwa Marekani, na nchi nyingi duniani.

Kujitenganisha na China

Utandawazi ulikuwa tayari umekabiliwa na tishio la uwepo wake wakati Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipoanzisha vita yva kibiashara na China mwaka 2018, na kuchochea ulipizaji kisasi baina ya nchi hizi mbili kwa njia ya utozaji kodi.

Rais Donald Trump (AP Foto/Alex Brandon, archivo)
Rais Donald Trump (AP Foto/Alex Brandon, archivo)

Mrithi wake, Joe Biden, alianzisha ulazima wa “kununua vilivyotengenezwa Marekani” katika mpango wake wa uwekezaji mpana ili “kuijenga tena Marekani.”

“Tutanunua vilivyotengenezwa Marekani ili kuhakikisha kila kitu kuanzia ujenzi wa uwanja wa ndege mpaka uzalishaji chuma kinachotumika kutengeneza vizuizi vya barabara kuu vinatengenezwa Marekani,” alisema katika hotuba yake ya hali ya kitaifa.

Rais wa Marekani Joe Biden (AP Photo/Evan Vucci)
Rais wa Marekani Joe Biden (AP Photo/Evan Vucci)

Dhana moja ambayo ilitokana na miaka ya utawala wa Trump ilikuwa “kutenganisha”—fikra ya kutenganisha uchumi wa Marekani na China.

Hofu hiyo haijaondoka, hasa wakati China ikikataa kuilaani Russia kwa uvamizi wake ilioufanya Ukraine.

Marekani imeutahadharisha uchumi mkubwa wa pili duniani utakabiliwa na “adhabu” iwapo itatoa msaada wa vifaa kwa Russia inayoendesha vita huko Ukraine.

China tayari ina masuala yenye utata na nchi za Magharibi, kama vile suala la Taiwan, demokrasia inayojitawala ambayo Beijing imeapa kuitawala siku moja, ikibidi hata kwa nguvu.

FILE PHOTO: Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa na Rais wa China Xi Jinping walipokutana Brasilia, Brazil November 13, 2019. Sputnik/Ramil Sitdikov/Kremlin via REUTERS .
FILE PHOTO: Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa na Rais wa China Xi Jinping walipokutana Brasilia, Brazil November 13, 2019. Sputnik/Ramil Sitdikov/Kremlin via REUTERS .

“Hivi sasa siyo katika maslahi ya China kuingia katika ushindani na nchi za Magharibi,” alisema Xiaodong Bao, Meneja katika kampuni inayosimamia samani ya Edmond de Rothschild.

Lakini vita vya Ukraine ni fursa kwa China kupunguza utegemezi wake kwa dola ya Marekani. Jarida la The Wall Street limeripoti kuwa Beijing iko kaitka mazungumzo na Saudi Arabia kununua mafuta kwa kutumia yuan badala ya dola.

“China itaendelea kutengeneza misingi yake kwa ajili ya siku za usoni,” Bao alisema. “Kujitenganisha kifedha kunaongezeka.”

Chanzo cha habari hii ni Shirika la Habari la AFP

XS
SM
MD
LG