Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 23:00

Moto wa msituni waua watu 26 Algeria


Mwanaume huyu anatizama moto wa msituni karibu na eneo la Larbaa Nath Irathen, kilomita 100 mashariki mwa mji mkuu wa Algeria, Algiers, Agosti 11, 2021.
Mwanaume huyu anatizama moto wa msituni karibu na eneo la Larbaa Nath Irathen, kilomita 100 mashariki mwa mji mkuu wa Algeria, Algiers, Agosti 11, 2021.

Watu 26 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika moto wa msituni katika wilaya 14 za kaskazini mwa Algeria Jumatano, waziri wa mambo ya ndani amesema

Waziri wa mambo ya ndani wa Algeria Kamel Beldjoud ameiambia televisheni ya taifa kwamba watu 24 wamepoteza maisha katika moto huko El Tarf, karibu na mpaka na Tunisia, pamoja na wengine wawili waliokufa mapema Jumatano huko Setif.

Idara ya ulinzi wa raia huko Setif imesema wanawake wawili, mama mwenye umri wa miaka 58 na binti yake mwenye umri wa miaka 31”, walifariki katika mji huo wa Setif.

Katika wilaya ya Souk Ahras, mbali zaidi upande wa mashariki karibu na mpaka wa Algeria na Tunisia, watu walionekana wakikimbia makazi yao huku moto ukitanda kabla ya helikopta za kuzima moto kupelekwa huko.

Ripoti ya awali ilisema watu wanne waliungua huko Souk Ahras na wengine 41 walikuwa na matatizo ya kupumua, maafisa wamesema. Ripoti za vyombo vya habari zimesema wakazi 350 walihamishwa.

Tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti, mioto 106 ilizuka nchini Algeria, ikiharibu zaidi ya hekta 2,500 za misitu.

XS
SM
MD
LG