Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:54

Moto na milipuko zaidi yatokea Brazaville


Wafanyakazi wa uwokozi wanasema ni hatari kuingia katika eneo ambalo kulitokea milpuko Jumapili katika mji mkuu wa Congo, Brazaville.

Wazima moto na wafanyakazi wa dharura katika mji mku wa Congo, Brazaville wanajaribu kuzuia moto kuenea na kufika karibu na ghala nyingine ya silaha iliyoko karibu mita 100 kutoka ghala lililolipuka Jumapili.

Maafisa wa serikali wanasema watu 146 wamefariki kutokana na mlipuko huo, lakini wafanyakazi wa afya wanasema idadi ya waliofariki imezidi 200 na walojeruhiwa ni zaidi ya 1,500.

Mashahidi wanaripoti kutokea milipuko midogo midogo Jumatatu, na maafisa wa kijeshi wananukuliwa wakisema kwamba kuna baadhi ya mizinga ambayo haikripuka. Hata hivyo msemaji wa jeshi Kanali Robert Obargui amewahakikishia wakazi kwamba "hali ya mambo inadhibitiwa."

Maelfu ya wakazi walimiminika katika barabara za BrazavilleSassou-Nguesso kuwahimiza kurudi katika nyumba zao, na kutangaza amri ya kutotoka nje usiku na kufunga wilaya ya mashariki ya Mpila ambako mlipuko ulitokea.

Kiongozi huyo alionekana kwenye televisheni ya taifa TeleCongo, akiwatembelea wagonjwa katika hospitali iliyofurika na waliojeruhiwa.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika aliyetembelea karibu na eneo la ajali anasema kuna uharibifu mkubwa na inahofiwa kwamba kuna watu walozkwa chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Maafisa wa serikali ya Congo wametoa wito wa msaada kutoka Jumuia ya Kimataifa baada ya kukutana na wanadiplomasia wa Marekani na Ufaransa siku ya Jumatatu.

XS
SM
MD
LG