Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:56

Morocco yaweka historia mpya ya kombe la dunia


Mchezaji wa Morocco, Achraf Hakimi akishangilia baada ya kufunga penalti ya ushindi katika mikwaju ya penalti wakati Morocco ikitinga robo fainali.REUTERS
Mchezaji wa Morocco, Achraf Hakimi akishangilia baada ya kufunga penalti ya ushindi katika mikwaju ya penalti wakati Morocco ikitinga robo fainali.REUTERS

Timu ya Morocco imefanikiwa kuweka historia kwa kuingia robo fainali kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia baada ya kuwashangaza miamba ya soka duniani Spain kwa kuwafunga kwa njia ya penati bao 3-0 katika uwanja wa Education City Al- Rayyan Qatar.

Hii ni baada ya baada ya kucheza dakika 120 ikiwa ni nyongeza baada ya timu hizo kutoka sare 0-0 ndani ya dakika 90 za mchezo huo.

Achraf Hakimi alifunga penalti ya ushindi kwa timu yake huku mashabiki wa Morocco wakishangilia kwa hali ya juu wakikumbatiana na kurukaruka pamoja na marafiki na familia.

Wakati huo huo nje ya uwanja, mamia ya watu walikusanyika na kuimba nyimbo za kitaifa, wakipiga picha za furaha na bila kutaka kuondoka uwanjani. Mechi hiyo ilionekana kama mchezo wa nyumbani kwa Simba wa Atlas huku wafuasi wao ambao ni wengi sana nchini Qatar wakiwazidi mashabiki wa Uhispania.

Katika eneo la Souq Waqif ambalo ni maarufu kwa mashabiki hao kukutana mashabiki wa Morocco , Ureno, Tunisia na nchi nyingine za kiarabu walijaa na kuimba nyimbo na kupiga tarumbeta za kushangilia timu ya Morocco.

“Tuna furaha kubwa kupata ushindi dhidi ya Spain , ni muda mrefu sana hatujaweza kufika hatua kama hii tumefurahi sana kuwa hapa na tuna fahari kubwa na timu yetu ya taifa na inshalaah katika mchezo ujao dhidi ya Ureno tutacheza kwa nguvu zetu zote tumefurahi sana tunachohitaji ni kushinda tu mchezo ujao” alisema Hamid kutoka Morocco.

Biashara katika eneo la Souq Waqif zilendelea kushamiri huku migahawa na maduka yakiendelea kuwahudumia mashabiki hadi saa za mapema Jumatano alfajiri.

Sasa timu ya Morocco itamenyana na Ureno katika robo fainali siku ya Jumamosi.

Ureno yaweka historia yaipa kipigo Uswisi

Nayo timu ya Ureno imetoa onyo kali baada ya kuiangusha Uswisi kwa mabo 6-1 na kuingia robo fainali kwa kishindo katika uwanja wa Kimataifa wa Lusail Doha.

Mshambuliaji Goncalo Ramos aliyecheza badala ya Christiano Ronaldo ambaye alikuwa na hati hati ya kutokucheza kutokana na mvutano na kocha wake. Lakini kicha alipoulizwa alisema huo ni mvutano wa ndani na wataumaliza wenyewe. Ila iulitajwa kutokea kutokana na Ronaldo kukasirishwa na kitendo cha kocha wake kumtoa katika mchezo uliopita na yeye hakutaka kutoka. Lakini mbadala wake huyo alionyesha makali yake baada ya kupachika mabao 3. Ramos alifunga bao la kwanza katika dakika ya 17.

Naye beki mkongwe Kepler Laveran de Lima Ferreira maarufu kama Pepe ambaye atafikisha miaka 40 mwezi wa pili aliifungia Ureno bao la pili na hivyo kuweka rekodi ya kuwa mfungaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga bao katika awamu ya mtoano katika historia ya Kombe la Dunia.

Mshambuliaji Ramos alifunga tena baada ya kipindi cha mapumziko.

Alikamilisha ‘hat trick’ yake baada ya mlinzi Raphaël Guerreiro kuifungia Ureno bao la nne naye Manuel Akanji akaifungia Uswissi bao la kufutia machozi. Jedwali la Robo fainali limekamilika ambapo ni kama ifuatavyo:

Croatia itapambana na Brazil Desemba 9.

Uholanzi na Argentina Desemba 9.

Morocco na Ureno Portugal December 10.

Uingereza na Ufaransa Desemba 10.

XS
SM
MD
LG