Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 04:37

Morocco yaitaka Russia kuhakikisha kesi ya haki kwa raia wake aliyehukumiwa kifo


Rais wa Russia Vladimir Putin akizungumza kupitia video kwenye hafla ya uzinduzi wa vituo vipya vya huduma ya afya mjini St Petersburg, June 18, 2022. Picha ya AP
Rais wa Russia Vladimir Putin akizungumza kupitia video kwenye hafla ya uzinduzi wa vituo vipya vya huduma ya afya mjini St Petersburg, June 18, 2022. Picha ya AP

Tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini Morocco imewataka viongozi wa Russia kuhakikisha "kesi ya haki" inafanyika kwa kijana raia wa Morocco aliyekata rufaa dhidi ya hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama inayounga mkono Russia nchini Ukraine.

Brahim Saadoun, raia wa Morocco aliyezaliwa mwaka 2000, alipewa adhabu ya kifo tarehe 9 Juni yeye na wanaume wawili raia wa Uingereza na mahakama ya jimbo la Donetsk, mashariki mwa Ukraine lililotangaza kujitenga.

Watatu hao walishtumiwa kuwa mamluki wa Ukraine kufuatia uvamizi wa Russia dhidi ya jirani yake.

Amina Bouayach, mwenyekiti wa Baraza la kitaifa la haki za binadamu ( CNDH), aliwasiliana na kamishna mkuu wa haki za binadamu katika serikali ya Russia, chanzo kutoka baraza hilo la haki za binadamu la Morocco kimeiambia AFP Jumapili.

Aliitaka taasisi hiyo ya haki za binadamu ya Russia "kuchukua hatua zinazohitajika kuhakikisha kesi ya haki kwa Brahim Saadoun wakati wa rufaa yake," chanzo hicho kimesema.

Taher Saadoun, baba wa mtuhumiwa, amesema mwanawe, ambaye alipata uraia wa Ukraine mwaka 2020, sio mamluki, akimtaja badala yake "kuwa muathirika wa upotovu".

Lakini Dmytro Khrabstov, rafiki wa Saadoun mwenye umri wa miaka 20, amesema raia huyo wa Morocco alijiunga na jeshi la Ukraine mwaka jana, akiwaambia marifiki zake kwamba anataka kufa kama shujaa.

XS
SM
MD
LG