Mabao ya Morocco yalifungwa na Hakim Ziyech katika dakika ya 4 na na En -Nesyri katika dakika ya 23.
Wakati bao la Canada lilifungwa na Nayef Aguerd katika dakika ya 40
Morocco kwa mara ya mwisho kufanikiwa kuingia raundi ya pili ya michuano ya kombe la dunia ilikuwa mwaka 1986.
Hivi sasa washabiki wa Morocco walikuwa na furaha kubwa kwa timu yao kuandika historia kwa kufanikiwa tena kuingia raundi ya pili baada ya miaka 37.
Japan yaiangusha Spain na kuingia raundi ya pili
Michuano ya kombe la Dunia nchini Doha inaendelea kuonyesha mshangao na maajabu baaada ya Japan kuangusha kigogo kingine kwa kuifunga Spain bao 2-1 katika uwanja wa Khalifa International.
Walikuwa ni Doan Ritsu na aliyepachika bao la kwanza katika dakika ya 48 na Ao Tanaka alipachika bao la pili dakika 3 baadaye na bao pekee la Spain lilifungwa na Alvaro Morata katika dakika ya 10.
Sasa Japan inaungana na Morocco na timu nyingne ikiwa imeongoza kundi F na kuingia raundi ya pili na katika raundi hiyo Japan itakwaana na Croatia.
Wakati timu ya Morocco itamenyana na Spain.
Ujerumani na Costa Rica nje
Timu ya taifa ya Ujerumani pamoja na imeifunga timu ya Costa rica bao 4-2 lakini pamoja na ushindi haikutoshakubaki mashindanoni.
Imemaliza kundi E ikiwa na pointi 4 sawa na Spain lakini Spain imejiwekea kibindoni magoli mengi ya kufunga.
Ujerumani kwa mara ya pili mfululiozo inatolewa katika hatua ya kwanza haya pia yalitokea ilipokuwa huko Russia 2018.
Je Ghana italipiza kisasi?
Na siku ya Ijumaa timu ya Ghana Black Stars itatupa karata yake ya mwisho dhidi ya Uruguay katika mchezo unaongojewa kwa hamu kubwa.
Itakumbukwa Ghana ilikosa nafasi ya kucheza nusu fainali baada ya Luis Suarez wa Uruguay kuzuia mpira na mkono wa shuti la Asamoah Gyan lilikuwa likienda wavuni mwaka 2010 na kupelekea mchezaji huyo kupewa kadi nyekundu na Ghna kupewa penati ambayo Asamoah Gyan alikosa na kupelekea Ghana kutolewa katika michuano hiyo.
Nayo timu ya taifa ya Ureno ikiongozwa na Ronaldo itavaana na Korea Kusini katika mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa utakuwa mkali.
Cameroon kuvaana na Brazil
Nao wawakilishi wengine wa Afrika Cameroon wanapambana na Brazil katika mechi ya kundi G Ijumaa.
Vijana wa Cameroon wanahitaji ushindi ili kuweza kusonga mbele katika kundi hili ambalo Brazil tayari imeshakata tiketi ya kuingia raundi ya pili.
Nayo timu ya Serbia inapambana na Uswissi ambapo wote wanahitaji ushindi ili kusonga mbele kama wakitoka sare na Cameroon akashinda basi atakuwa na nafasi ya kusonga mbele.