Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:08

Morocco na Israel zakubaliana kuimarisha ushirikiano wa kijeshi


Abdelhamid Addou, mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege la Morocco, akitoa taarifa baada ya ndege ya kwanza ya Morocco aina ya Boeing kutua kwenye uwanja wa ndege wa Israel wa Ben Gurion, Machi 13, 2022
Abdelhamid Addou, mwenyekiti wa bodi ya shirika la ndege la Morocco, akitoa taarifa baada ya ndege ya kwanza ya Morocco aina ya Boeing kutua kwenye uwanja wa ndege wa Israel wa Ben Gurion, Machi 13, 2022

Jeshi la Morocco Jumanne limesema limekubaliana na Israel kuimarisha ushirikiano wa kijeshi ikiwemo katika sekta za ujasusi na usalama wa mitandaoni, kufuatia mikutano kuhusu ulinzi iliyofanyika mjini Rabat.

Nchi hizo mbili zilikubaliana kuimarisha ushirikiano na kuupanua kwenye sekta nyingine, zikiwemo ujasusi, ulinzi wa anga na vita dhidi ya udukuzi wa mtandaoni, jeshi la Morocco limesema katika taarifa.

Tangazo hilo la Jumanne linafuatia mkutano wa kwanza wa kamati ya ufuatiliaji kwa ajili ya ushirikiano kwenye sekta ya ulinzi kati ya Morocco na Israel uliofanyika katika mji mkuu wa Morocco, Rabat.

Mkutano huo wa siku mbili ulichunguza ushirikiano wa kijeshi ikiwemo katika nyanja ya kiufundi, mafunzo na upatikanaji na uboreshaji wa vifaa.

Nchi hizo mbili zilirasimisha uhusiano mwaka wa 2020, kufuatia makubaliano kama yale yaliyofikiwa kati ya Israel na Umoja wa falme za kiarabu na Bahrain.

Hii ni baada ya Marekani kutambua mamlaka ya Morocco kwenye eneo linalozozaniwa la Western Sahara, ili Morocco nayo ianzishe tena uhusiano na Israel.

XS
SM
MD
LG