Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 16:23

Moreno Ocampo

Kiongozi wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu Bw.Louis Moreno Ocampo anaendelea na ziara ya siku 5 huko nchini Kenya ambapo tayari amekutana na zaidi ya waathiriwa 30 waliokumbwa na ghasia na maafa ya uchaguzi mkuu uliopita.

Na pia alikutana na baadhi ya Mawaziri, maafisa wakuu wa serikali na maafisa wa usalama wa taifa nchini humo.

Akizungumza na vyombo vya habari na raia wa Kenya walioathiriwa na ghasia na mauaji baada ya uchaguzi mkuu uliopita alisema anaendelea na uchunguzi wake bila kutegemea serikali au mashirika ya kibinafsi .

Ameongeza kuwa shabaha yake si kuchunguza matatizo ya kisiasa yaliyotokea nchimi humo wakati wa uchaguzi mkuu uliopita bali lengo lake ni kuchunguza makosa ya jinai.

Lakini baadhi ya wanasiasa kutoka maeneo ya Rift Valley wanadai kwamba washukiwa wakuu wa ghasia hizo ni rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga ambao aliongea nao kwa mara ya kwanza alipoingia nchini humo.

Lakini Ocampo anasema lengo lake kwenda Kenya ni kusikiliza madhila yaliyowapata waathiriwa wa ghasia hizo za uchaguzi.

XS
SM
MD
LG