Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:26

MONUSCO na FARDC wanawasaka waasi huko Beni nchini DRC


Kikosi cha ulinzi wa amani cha MONUSCO wakiwa katika doria kwenye wilaya ya Beni huko DRC
Kikosi cha ulinzi wa amani cha MONUSCO wakiwa katika doria kwenye wilaya ya Beni huko DRC

Jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa- MONUSCO katika kikosi chake maalum kutoka Tanzania kinaendelea na msako wa kuwapata waasi wa ADF katika misitu ya Beni nchini jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC kwa kushirikiana na jeshi la Congo AFRDC .

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:20 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa sauti ya Amerika-VOA aliyeko huko Beni alisema kwamba kikosi cha MONUSCO na AFRDC vipo msituni kwa takribani siku 10 katika operesheni ya kuwasaka waasi hao wanaoshukiwa kufanya mauaji katika eneo hilo.

Vikosi hivyo kwa pamoja vinaendesha operesheni kwenye maeneo ya Kokola ambayo yanaripotiwa kwamba waasi walifanya mauaji majira ya asubuhi kwa saa za huko.

XS
SM
MD
LG