Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 14:10

Monastir ya Tunisia mabingwa wanyakua ubingwa BAL


Jean Jacques wa REG akipiga chenga wakati wa mchezo dhidi ya US Monastir ya Tunisia.
(Picha na Pape Emir/NBAE via Getty Images)
Jean Jacques wa REG akipiga chenga wakati wa mchezo dhidi ya US Monastir ya Tunisia. (Picha na Pape Emir/NBAE via Getty Images)

Timu ya US Monastir ya Tunisia wameibuka mabingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika Msimu wa 2 baada ya ushindi wa jumla ya pointi 83-72 dhidi ya Petro de Luanda ya Angola katika mchezo wa fainali Uwanja wa Kigali Arena, nchini Rwanda Jumamosi.

Baada ya kushindwa na Zamalek ya Misri katika Fainali ya Msimu wa kwanza, timu ya US Monastir ilikabiliana na timu yenye nguvu ya Petro katika Fainali za Msimu wa 2 huku Waangola hao wakitangulia mapema katika Mchezo huo lakini Dixon alijibu kwa pointi tatu kutoka kwenye kona ya uwanja.

Lahyani alichukua pasi kutoka kwa Diabate na akaweka ndani danki ya mkono mmoja na kuiweka Monastir karibu katikati ya kota ya pili.

Concalves wa Petro alijibu kwa pointi tatu na kuwaweka Waangola mbele katika mchezo huo.

Lakini Monastir walijibu kwa pointi tatu zao kutoka kwa Dixon na kupunguza tofauti ya magoli mapema katika kota ya nne.

Correia alifunga tena ili kudumisha uongozi wa Petro mwishoni mwa kota ya nne.

Majok alijibu kwa Monastir kwa dunk ya mkono mmoja baada ya pasi kutoka kwa Dixon.

Majok alikuwa shujaa tena kwa Monastir baada ya kuzuia mpira dhidi ya Moreira huku muda ukizidi kuyoyoma kwa timu ya Angola.

Hatimaye mchezo uliisha kwa Tunisia kushinda kwa jumla ya pointi 83-72.

XS
SM
MD
LG