Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 18:34

Mcheza filam wa Tanzania Monalisa atoa wito kwa wawekezaji kutupia jicho filam za Bongo.


Monalisa
Monalisa

Mcheza filam maarufu wa Tanzania aliyeshinda tuzo ya filam ya mwigizaji bora wa kike huko Ghana Aprili mwaka huu katika tuzo za African Prestigous Awards Yvonne Cherrie au maarufu kama Monalisa anasema alivutiwa na mama yake kuingia katika filam nchini humo.

Alipotembelea Jukwaa la Vijana la VOA ameeleza changamoto za wacheza filam nchini humo si sawa na zile za wanamuziki. Kwasababu inachukua watu wengi na gharama kubwa .

Na faida ipo lakini akiongeza si ile wanayotarajia akisema kwa Tanzania bado lakini anaamini watafika kwani bado sekta hiyo ni changa.

Ametoa wito kwa wawekezaji kwenda kuwekeza kwenye sekta ya filam nchini humo, kwasababu anaamini watranzania wanapenda kazi zao na kuna nafasi kubwa ya maendeleo katika sekta hiyo.

Tuzo alizopata anasema zina maana kubwa sana kwake na alipopata tuzo yake ya kwanza ya ZIFF alitoa machozi na ni fahari kubwa kwake hali kadhalika tuzo aliyoipata Ghana.

Amewataka wanawake kujiamini na kuwekeza nguvu na akili katika kile wanachotaka kufanya na wasiskilize kelele za nje bila kusahau kumshirikisha Mungu katika maisha aliongeza.

XS
SM
MD
LG