Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:50

Afungwa miaka 20 kwa madai ya ugaidi Kenya


terror suspect found guilty
terror suspect found guilty

Mahakama moja ya Mombasa, Kenya, imempa adhabu ya miaka 20 gerezani mwalimu mmoja wa madras baada ya kumkuta na hatia ya kuchochea wanafunzi wa shule ya msingi kuwa na siasa kali.

Mwalimu huyo Samuel Wanjala Wabwile ambaye pia anajulikana kama Salim Mohamed, alikutwa na hatia ya kutumia darasa lake kuwachochea wanafunzi kuingia katika siasa kali ambazo zinavutia pia vitendo vya kigaidi.

Katika huku yake hakimu Diana Mochache alisema kuwa Wabwile alitumia akili changa ya watoto kuwatia mawazo ya kukubali sera kali na hivyo kuhatarisha maisha ya watoto hao na jamii kwa jumla.

Kabla ya kuwa mwalimu wa madras Wabwile alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Maseno mjini Kisumu ambako alifukuzwa kwa sababu ambazo hazijafahamika.

XS
SM
MD
LG