Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:13

Mohammed Morsi aapishwa kuwa rais wa Misri


Morsi ala kiapo nje ya mahakama ya kikatiba

Mohammed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood ameapishwa kama rais mpya wa Misri Jumamosi na hivyo kuadhimisha enzi mpya katika historia ya taifa hilo kwa kuchaguliwa rais wa kwanza wa kiraia. Bwana Mosri alikula kiapo katika sherehe zilizofanyiwa nje ya mahakama ya kikatiba. Aliapa kutii katiba ya Misri. Morsi anaingia madarakani baada ya rais Hosni Mubarak kutimuliwa katika maandamano ya umma mwaka jana. Rais huyo mpya pia amehutubia taifa la Misri kutoka mji mkuu wa Cairo. Sherehe za kuapishwa kwakwe zimefanyika siku moja baada ya kuhutubia maelfu ya wafuasi wake waliojazana katika uwanja wa Tahrir Square kupinga baraza la utawala la kijeshi nchini humo. Alisema raia wa Misri kote nchini humo na wale walio nje pamoja na wale waliomwaga damu yao katika vuguvugu la mapinduzi ya kiutawala wamefungua njia mpya ya uhuru. Aliwashukuru Wamisri pia kwa kumpa nafasi ya kuongoza taifa hilo. Awali Morsi aliapa kula kiapo cha madaraka nje ya majengo ya bunge lakini baraza la kijeshi likasema ataapishwa nje ya mahakama ya kikatiba kwa sababu baraza la wawakilishi bungeni na ambalo lilikuwa na wabunge wengi wa chama chake cha Muslim Brotherhood llilikuwa limevunjwa. Baadhi ya wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanasema mgongano huo wa mawazo huenda ukaibuka na kuwa mvutano tena baina ya chama chake cha Brotherhood na baraza hilo la kijeshi.

XS
SM
MD
LG