Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 12:53

Kasi ya kuleta utawala bora barani Africa yapunguka


Washiriki kwenye mkutano wa taasisi ya Mo Ibrahim.
Washiriki kwenye mkutano wa taasisi ya Mo Ibrahim.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:45 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Maendeleo katika utawala bora kote barani Afrika yanadumaa, hiyo ni kwa mujib wa takwimu za hivi karibuni zilokusanywa na taasisi isiyo ya kiserikali ya wakfu ya Mo Ibrahim. Taasisi hiyo inaeleza kwamba pamoja na wasi wasi wa ukosefu wa uhuru wa kisiasa, ni nchi kadhaa tu ambazo zinaonyesha maendeleo kidogo.

Kipimo cha taasisi ya Mo Ibrahim kinaeleza kuwa kina mkusanyo wa kutosha na wa kina wa takwimu juu ya utawala barani Afrika. Kila mwaka wachambuzi wanapima kila nchi kwenye vyenzo kama vile mandhar yake ya kibiashara, uwajibikaji wa viongozi wake, na sheria juu ya ghasia dhidi ya wanawake.

Wakati wa kuzinduliwa kwa ripoti yake mpya ya kila mwaka, muasisi wa taasisi, Mo Ibrahim, alisema kwamba mwenendo jumla mnamo miaka minne ilopita inazusha wasiwasi.

Nchi takriban 21 zimeshuhudia natija zao jumla za utawala zimeanguka tangu mwaka 2011.

Lakini mwenendo huo unaficha maendeleo makubwa katika baadhi ya nyanja. Afya na elimu zimeboreka kote barani Africa. Ibrahim anasema Ivory Coast, ambayo inatarajiwa kufanya uchaguzi baadae mwezi hu, ilionyesha maenedeleo makubwa zaidi kiujumla.

Ibramim anasema, Cote de Voire imefanya vyema katika kila nyanja ya utawala. Lakini lazima ukumbuke kuwa Cote de voire inatoka kutoka mzozo. Lakini pia kuna baadhi ya nchi ambazo hazitoki kwenye mzozo, kama vile Rwanda , Morocco, Togo, Kenya, nchi hizi zina utawala amabo zinalenga sana katika maenedeleo na zinafanikiwa.

Mizozo inayoendelea huko Somalia, Sudan kusini na Jamhuri ya Africa ya kati, imemaanisha nchi hizo ziko chini katika orodha.

Vipimo katika utawala wa kiuchumi vinaonyesha kuanguka kwa kiasi kikubwa. Wachambuzi wanasema nchi kadhaa za kiafrika zimeathirika kwa sababu ya kuanguka kwa bei za bidhaa katika miaka ya hivi karibuni.

Nazo nchi zenye ufanisi zina mchanganyiko wa harakati za kiuchumi , anasema rais wa zamani wa benki ya maendeleo ya Africa ADB, Bw. Donald Kaberuka, alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi huko mjini London.

Kaberuka anasema, jambo linalofanana kati ya nchi hizo ni kwamba hazitegemei bidhaa za matumizi ya kila siku. Kwa hiyo kumekuwepo na mambo mengine yalofanyika, ambayo ni kuongeza uwekezaji, pili kuongezeka kwa matumizi ya ndani, na tatu ni ukuwaji wa biashara ya kikanda usopewa umuhimu.

Tassisi ya Mo Ibrahim inaeleza kuwa lengo la orodha hiyo ni kuondowa tesi juu ya utawala na kuwawezesha raia wa kawaida wa Afrika kuwawajibisha wale walio uwongozini.

XS
SM
MD
LG