Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:31

Mmoja wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Rwanda akamatwa Congo


wanajeshi wa Congo
wanajeshi wa Congo

kiongozi huyo wa zamani wa kundi la wanamgambo la wahutu Bernard Munyagishari alikamatwa kufuatia operesheni za jeshi huko Kivu ya Kaskazini.

Maafisa wa usalama wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamemtia nguvuni mmoja wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994.

Msemaji wa jeshi la Congo Meja Olivier Hamili amesema kiongozi huyo wa zamani wa kundi la wanamgambo la wahutu Bernard Munyagishari alikamatwa kufuatia operesheni za jeshi huko Kivu ya Kaskazini.

Munyagishari alikuwa anasakwa kwa tuhuma za makosa ya mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu na ubakaji.

Aidha Meja Hamili amesema hivi sasa anashikiliwa na mamlaka za usalama huko Goma akihojiwa dhidi ya tuhuma hizo.

Bado haijafahamika kama Munyagishari aliyekuwa kichocheo cha mauwaji ya watusti wanaokadiriwa kufikia laki nane na wahutu wenye msimamo wa kadri wakati wa mauaji ya halaiki kwa zaidi ya kipindi cha mwezi mmoja, kama atashitakiwa katika mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda iliyoko Arusha nchini Tanzania au La.

Hivi karibuni maafisa wa usalama wa Kivu Kaskazini walianzisha operesheni kabambe zikisimamiwa na Gavana wake Juliuan Paluku kuhamasisha wananchi kwa kushirikiana na jeshi kusaidia katika harakati za kutimuwa waasi wa Rwanda wa –FDLR.

Marekani iliahidi dola milioni 5 kwa yeyote atakepelekea kukamatwa kwa Munyagishari.

XS
SM
MD
LG