Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:05

M'marekani mwenye asili ya Somalia afanya shambulizi la bomu


Eneo la shambulizi la bomu mjini Mogadishu Oktoba 18, 2011
Eneo la shambulizi la bomu mjini Mogadishu Oktoba 18, 2011

Kijana raia wa Marekani ajitoa mhanga na kushambulia walinda amani Mogadishu

Kundi la wanamgambo wa al-Shabaab nchini Somalia linasema raia wa Marekani alikuwa mmoja kati ya watu wawili waliojitoa mhanga na kufanya shambulizi la bomu dhidi ya kituo cha walinda amani wa Umoja wa Afrika katika mji mkuu Mogadishu. Radio inayounga mkono wanamgambo wa al-Shabaab pamoja na tovuti, zimemtambulisha mshambuliaji huyo raia wa Marekani mwenye asili ya Somalia kama kijana kwa jina Abdisalam. Radio hiyo inasema kijana huyo alihamia Marekani akiwa na umri wa miaka miwili. Maafisa wa Marekani hawajathibitisha madai hayo ingawa kumekuwa na baadhi ya raia wa Marekani wenye asili ya Somalia wanaoaminika wamekwenda Somalia kujiunga na wanamgambo hao. Jumamosi watu wawili walijitoa mhanga na kufanya shambulizi la bomu nje ya kituo cha walinda amani wa Umoja wa Afrika mjini Mogadishu. Haikubainika mara moja ni walinda amani wangapi waliouawa katika shambulizi hilo lakini al-Shabaab inadai ni dazeni kadha. Al-Shabaab wanapigana kuiangusha serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ili wabuni taifa la kiislam. Lakini kundi hilo la wanamgambo limepata pigo kutoka kwa serikali ya Somalia pamoja na walinda amani wa Umoja wa Afrika katika miezi ya karibuni ingawa bado wanadhibiti maeneo makubwa ya kusini na katikati mwa Somalia.

XS
SM
MD
LG