Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:10

Mlipuko wa bomu wauwa watu kadhaa Somalia


Wanamgambo wa al-Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulizi kadhaa mjini Mogadishu, Somalia.
Wanamgambo wa al-Shabaab wamekuwa wakifanya mashambulizi kadhaa mjini Mogadishu, Somalia.

Mashahidi na maafisa walisema watu wasiopungua watano walifariki Jumatano baada ya mlipuko mmoja kutokea kwenye soko la mifugo katika mji wa Afgoye, kilomita 30 magharibi mwa Mogadishu.

Wakazi katika eneo wameiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba wanajeshi wawili wa serikali na raia watatu walikufa katika mlipuko unaoaminika unatokana na vifaa ambavyo viliwekwa katika soko. Watu wane wengine walijeruhiwa. Maafisa wanaamini kundi la wanamgambo la al-Shabaab lilifanya shambulizi hilo.

Mapema Jumatano, watu wawili walipigwa risasi na kufariki mjini Mogadishu shambulizi lilifanywa na wanamgambo wa al-Shabaab. Mmoja wa waathirika ametambuliwa kama Dr.Liban Osman Elmi, mpwa wa Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud. Muathirika wa pili ni Abdulkadir Mohamud Yabarow, mfanyakazi wa wizara ya sheria.

Kundi la al-Shabaab linadai kuhusika kwa mauaji hayo.

XS
SM
MD
LG